Micah 7:8-9

Israeli Atainuka


8 aUsifurahie msiba wangu, ee adui yangu!
Ingawa nimeanguka, nitainuka.
Japo ninaketi gizani,
Bwana atakuwa nuru yangu.

9 bKwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake,
nitabeba ghadhabu ya Bwana,
mpaka atakaponitetea shauri langu
na kuithibitisha haki yangu.
Atanileta nje kwenye mwanga,
nami nitaiona haki yake.
Copyright information for SwhKC